Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) limekanusha taarifa za kuibiwa kwa kifaru cha jeshi zilizoripotiwa leo na gazeti la Dira na kusema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowowte huku likisisitiza ulinzi katika maeneo ya jeshi uko imara.
Akiongea na waandishi wa habari leo kukanusha habari hizo, msemaji wa jeshi hilo, Kanali Ngemela Lubinga amesema jeshi limesikitishwa sana na habari hizo za upotoshaji kwa kuwa zinachafua taswira ya jeshi na taifa kwa ujumla.
Amelitaka Gazeti la Dira kuomba radhi mara moja na wakishindwa kufanya hivyo hatua Kali na za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Post a Comment