Duterte kuapishwa Philippines leo
Duterte kuapishwa Philippines leo.
Meya mtata wa zamani wa jimbo la Davao nchini Philippines, Rodrigo Duterte, anakaribia kuapishwa kama Rais wa nchi hiyo masaa machache yajayo.
Duterte alishinda uchaguzi mkuu mwezi uliopita ambao aliahidi kupigana vita juu ya uhalifu uliokithiri nchini humo.
Katika kipindi cha miaka zaidi ya 20 kama Meya wa Davao,mji wa tatu kwa ukubwa nchini humo, Duterte aliunga mkono kuuawa kwa wahalifu katika jimbo lake jambo ambalo liliupunguza kwa kiasi kikubwa.
Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa maelfu ya watu waliuawa bila kufuata mchakato wa kisheria.
Post a Comment