Header Ads

Barcelona yashuka daraja

Related image

labu ya soka ya Barcelona B imetelemka daraja kutoka Ligi daraja la kwanza ya Hispania 
maarufu kama (Segunda División) hadi daraja la pili (Segunda B) baada ya kukubali sare ya 
0-0 na Albacete jana usiku.
Timu hiyo ya vijana ya Barcelona kwa misimu kadhaa imekuwa bora kiasi cha kufikisha alama za kupanda ligi kuu ya La Liga, lakini kutokana na kanuni kutoruhusu timu mbili zenye umiliki mmoja kucheza ligi moja, iliendelea kubaki 'Segunda División'.
Msimu huu mambo yameenda vibaya ambapo hadi sasa inashika nafasi ya 20 kati ya timu 22 ambazo zinacheza ligi daraja la kwanza maarufu kama Segunda División. Tayari timu hiyo imecheza mechi 41 kati ya 42 za msimu huu ikiwa na alama 44.

Mapema mwezi April Barcelona B, walimtimua kocha wao mkuu Gerard Lopez kutokana na matokeo mabovu na kumteua Francesc Xavier Garcia Pimienta ambaye ameshinda mechi 2 tu kati ya 5 alizocheza.
Timu tatu ambazo ziko katika hali nzuri ya kupanda hadi La liga msimu ujao ni Rayo Vallecano iliyopo kileleni na alama 76, Huesca yenye alama 75 katika nafasi ya pili na Sporting Gijón yenye alama 71 katika nafasi ya tatu.

No comments