Header Ads

Watoto 210 waachiwa huru na makundi wa wapiganaji Sudan Kusini


Image result for Watoto 210 waachiwa huru na makundi wa wapiganaji Sudan Kusini


Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watoto 200 wameachiwa huru na makundi ya wapiganaji katika taifa linalokumbwa na mzozo la Sudan Kusini. 

Naibu msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amewaambia wanahabari kuwa kuachiwa huru kwa watoto hao ni tukio la tatu la aina hiyo mwaka huu na hivyo kufikisha idadi jumla ya watoto walioachiwa huru na makundi ya wapiganaji kufikia 806.

Haq amesema wanatarajiwa watoto zaidi kuachiwa huru katika kipindi cha miezi michache ijayo. Watoto hao 210 wakiwemo wasichana watatu, walioachiwa huru Alhamisi wiki hii pamoja na famili zao watapewa chakula kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, mafunzo ya kiufundi na elimu.

TABORA YA VAMIWA

No comments