Wanaotaka kustaafu wapewa onyo
Katibu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), Bi. Winifrida Rutahindurwa amewaonya waalimu wanaofanya udanganyifu katika taarifa zao za kiutumishi kwa lengo la kujiongezea muda wa kuwepo katika utumishi wa umma licha ya kuwa umri wao wa kustaafu kwa mujibu wa sheria kufika.
Bi. Rutahindurwa ametoa kauli hiyo Mei 29, 2018 mjini Bagamoyo alipokutana na waalimu wakuu na wakuu wa shule za umma kutoka wilaya za Bagamoyo na Chalinze kwa lengo la kutoa elimu juu ya wajibu wao na kusema kuwa kuna wakati walimu walitakiwa kupeleka taarifa zao za kiutumishi kwa waajiri wao lakini baadhi yao walipeleka taarifa tofauti na zile walizojaza kwenye mikataba ya kazi wakati wa kuanza ajira.
"Kuna baadhi ya waalimu wanajifanya hawakumbuki walizaliwa mwaka gani wakati walijaza mikataba wakati wanaanza ajira na wengi wao wamebadilisha taarifa zao na kujipunguzia umri jambo ambalo ni kinyume na taratibu na sheria", amesema Bi. Rutahindurwa.
Aidha, Bi. Rutahindurwa amefafanua kuwa mwalimu atakapoandikiwa kibali cha kustaafu, TSC pamoja na mfuko wamifuko ya hifadhi ya jamii wanajikita zaidi kuangalia taarifa za mwalimu alizojaza awali wakati anaanza ajira yake na sio kutegemea taarifa za stakabadhi ya mishahara peke yake.
"Naomba muwaeleze walimu wote katika shule zenu kuwa utakapoandikiwa kibali cha kustaafu sisi tunaangalia zaidi taarifa zako ulizojaza wakati unaajiriwa na ukibainika umedanganya utachukuliwa hatua kwa kuwa umemwibia mwajiri", amesisitiza Bi. Rutahindurwa.
Kwa upande wao waalimu walionesha kupokea maelekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuondoa usumbufu kwa mwalimu pale anafuatilia masuala yake ya mafao mara baada ya kustaafu.
WENYE VITI WA MTAA MARUFUKU KUJIUSICHA NA KUUZA ARIDHI
Post a Comment