Header Ads

Yanga yakanusha kupotea kwa fedha




Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Msemaji wake Dismas Ten, umekanusha taarifa zilizoenea mitandaoni na katika baadhi ya vyombo vya habari zikieleza kuwa mapato ya fedha yaliyotokana na uuzaji wa kalenda na majarida yake zimeishia mifukoni mwa baadhi ya viongozi.

Ten ameeleza hayo akisema kuna baadhi ya watu waliokuwa viongozi wa Yanga wameamua kuanzisha kampeni ya chini kwa chini ili kuichafua klabu hiyo iliyopo mitaa ya Twiga, Jangwani Jijini Dar es Salaam.
Msemaji huyo amesema watu hao wamekuwa wakiichafua Yanga wakihitaji kurejea kwa ajili ya kuitumikia klabu japo imekuwa si rahisi kutokana na kukosa nafasi katika utawala uliopo hivi sasa.
Kufuatia taarifa hizo, Ten ameeleza kuwa hazina ukweli wowote na akiomba wadau wote wa Yanga kuzipuuza sababu hazina malengo chanya na uongozi uliopo pamoja na klabu kwa ujumla.
 Ajali Yaua Watu Wawili Pwani


No comments