Header Ads

Makanisa yavamiwa na kushambuliwa kwa mabomu


Watu waliojitoa mhanga wamevamia makanisa matatu nchini Indonsia na kuyalipua kwa mabomu.
Milipuko hiyo imetokea katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo wa Surabaya na kusababisha vifo vya watu 9, huku idadi hiyo ikitazamiwa kuongezeka.
Zaidi ya watu 13 wamepata majeraha, baadhi yao mabaya sana. Misururu ya milipuko hiyo ya mabomu yalifuatana.
Hakuna kundi lolote lilokiri kuhusika katika mashambulio hayo, lakini kundi linalojiita Jemaah Ansharut Daulah (JAD), ambalo lina uhusiano na kundi la wapiganaji wa kigaidi wa Islamic State, huenda lilihusika kwa mujibu ya Jeshi la polisi nchini humo.

No comments