Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 31.05.2018
Mourinho anamfuatilia Marko Arnautovic, Chelsea macho yao kwa Robert Lewandowski
Manchester United wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi wa kikosi cha West Ham Marko Arnautovic. The Hammers wananaweza kutaka malipo ya pauni £50m kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Australia. (Sky Sports)
Lakini West Ham inasema hawataki kumuuza mshambuliaji huyo msimu huu. (Evening Standard)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho alionekana katika mchezo wa kirafiki Jumatano baina ya Austria na Urusi , mchezo ambao aliucheza Arnautovic. (Vivaro News)
Chelsea wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji kutoka Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29 baada ya kutangaza kuwa anataka kuondoka Bayern Munich. (Mirror)
Liverpool inataka kumuuza mshambuliaji wao Mfaransa Nabil Fekir mwenye umri wa miaka 24 kwa Lyon kwa euro milioni 60m (Le Parisien)
Na Liverpool wanaye mlinda lango wa Barcelona Jasper Cillessen raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 29 kwenye orodha yake ya wachezaji wanaotaka kununua. (Mundo Deportivo)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Italia Jorginho, mwenye umri wa miaka 26, yuko tayari kujiunga na kikosi cha Manchester City kutoka Napoli baada ya kununuliwa kwa euro milioni hamsini baada ya kukubali mkataba wa miaka mitano na Man City. (La Gazzetta dello Sport)
Kocha wa timu ya Ufaransa Didier Deschamps amemshauri mshambuliaji wa safu ya mbele Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 27, aendelee kubaki Atletico Madrid badala ya kujiunga na Barcelona. (RMC Sport)
Arsenal wamekamilisha mipango ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati ya Ufaransa Yacine Adli mwenye umri wa miaka 17 kutoka kikosi cha Paris St-Germain. (Mirror)
Mshindi wa Kombe la Dunia akiwa na Brazil Ronaldo anataka kununua klabu ya Uhispania Real Valladolidkwa euro milioni 30. (O Globo)
Everton wanaweza kufufua tena azma yao ya kumtaka Mholanzi Patrick Van Aanholt, mwenye umri wa miaka 27 anayecheza katika safu ya ulinzi ya Crystal Palace (Daily Mail)
Newcastle wamepewa fursa ya kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati Joe Allen anayeichezea Stoke City akiwa na umri wa miaka 28. Anatokea Wales
Fulham watatakiwa kulipa karibu pauni milioni £20m kusaini mkataba na Mserbia Aleksandar Mitrovic anayeichezea Newcastle.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akicheza kwa mkopo katika Craven Cottage msimu uliopita na aliisaidia klabu hiyo kupanda daraja na kuingia Ligi ya Premia. (Evening Standard)
Justin Kluivert -mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa timu ya Uholanzi Patrick Kluivert - anaweza kubakia katika Ajax licha ya fununu kwamba anapanga kuhama. Kluivert mwenye umri wa miaka 19 winga wa Uholanzi amekuwa akihusishwa na timu za Manchester United na Tottenham. (Fox Sports - in Dutch)
Kluivert amekubali mkataba wa Roma, lakini bado hawajaafikiana juu ya malipo na wenzao wa Uholanzi juu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi . (Gianluca di Marzio - in Italian)
Mchezaji wa safu ya ulinzi Michael Dawson, mwenye umri wa miaka 34, amekubali kurejea Nottingham Forest kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mkataba wake na Hull kumalizika. (Daily Mail)
Southampton na Aston Villa wanamtaka mlinzi wa timu ya Ujerumani Tobias Pachonik.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa sasa yuko huru kwani bado hajasaini mkataba mpya na Carpi FC iliyopo katika Ligi ya pili ya Italia . (Turkish Football)
Post a Comment