Header Ads

Simba ya shindwa kufuta rekodi ya Yanga






Baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa msimu huu, huku wakimaliza ligi wakiwa na alama 69, rekodi zinaonesha wameshindwa kuvunja rekodi za Yanga katika msimu wa 2015/16.

Msimu huu Simba imeshinda mechi 20 pekee kati ya 30 ambazo ndio mechi za msimu mzima, ambapo Yanga katika msimu wa 2015/16 ilishinda mechi 22 kati ya 30 za msimu huo.
Simba pia imetoa jumla ya sare 9 msimu huu lakini wapinzani wao wa Jadi Yanga walifanikiwa kutoa sare 7 pekee kwenye msimu wao wa 2015/16 ambapo waliibuka mabingwa wa ligi. 
Kwa upande wa mabao ya kufunga Simba pia washindwa kufikia mabao 70 ya Yanga wakiishia mabao 62 pekee msimu huu. Kwenye mabao ya kufungwa Simba wamefanya vizuri ambapo wameruhusu mabao 15 tu lakini Yanga walikubali mabao 20.
Kwa upande wa alama Simba wameshindwa kufikia alama 73 za Yanga msimu huo wakiishia alama 69 pekee katika michezo yao 30. Msimu huu timu pekee iliyovunja rekodi ya alama ni Manchester City ambayo ilifikisha alama 100 na kuvunja rekodi ya alama 95 iliyowekwa na Chelsea msimu wa 2004/05. 

TABORA  YA OMBEWA MAFANIKIO


No comments