Header Ads

Wabunge hawafuati utaratibu"- Pius Msekwa



Sakata la matibabu ya Wabunge, Spika wa zamani wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa Wabunge hawafuati utaratibu kwa kufanya maamuzi yao binafsi.

Msekwa amefunguka hayo wakati akizungumza na eatv.tv na kusema kuwa kuna taratibu za matibabu kwa Wabunge na hairuhusiwi kutibiwa hospitali yoyote kwa uamuzi binafsi lakini wanashindwa kufuata miongozo hiyo na kuibua migogoro.
“Mbunge akiugua huwa anapelekwa hospitali ya serikali na endapo akitakiwa kuhamishwa hospitali atapewa rufaa na lazima bunge liwe na taarifa hakuna anayefanya maamuzi yake binafsi alafu anahitaji kulipwa”, amesema Msekwa.
Aidha, Msekwa ameongeza kuwa hakuna upendeleo kama ambavyo Kambi ya Upinzani Bungeni inavyodai na imekuwa hivyo tangu mwanzo kwa kuwa fedha zinazotumika ni za umma na zinataratibu zake.
Hayo yamejiri baadaya kuwepo kwa madai kuwa Wabunge wa upinzani hawapewi kipaumbele pindi wanapotakiwa kupatiwa matibabu.


mtaa wa mabatini uchafu umekidhili

No comments