Header Ads

Mkurugenzi mtendaji wa maji safi tabora kumsimamisha kazi

Image result for Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya sikonge Mkoani Tabora


Baraza la madiwani
wa  halmashauri ya wilaya ya sikonge
Mkoani Tabora limemwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo kumsimamisha
kazi Meneja wa mamlaka ya maji safi na Usafi wa Mazingira (SUWASA)  Eginia Benjamini Briton kwa tuhuma za ubadhifu
wa fedha za umma na Matumizi mabaya ya ofisi.

Maagizo hayo
yametolewa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mwalim Peter Nzalalila katika
kikao cha baraza la madiwani
kilichofanyika katika ukumbi wa chuo cha maendeleo ya jamii FDC Wilayani
humo.

Amesema kuwa
baraza hilo limeazimia kwa kauli moja
kumsima
misha kazi   meneja huyo
kutokana na kuwepo kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha za umma pamoja na matumizi
mabaya ya ofisi hali ambayo imekuwa ikipelekea hali ya upatikanaji wa maji
wilayani humo kuwa wakusuasua.
Akipokea maagizo
hayo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Daktari Simoni Ngatunga amesema
kuwa atatekeleza agizo hilo kwa kutumia kanuni,sheria na Taratibu kwa kuwa hana
mamlaka ya kutengua uteuzi wa bodi ya maji ambayo inateuliwa na Wizara ya maji
na Umwagiliaji

Nao baadhi ya
madiwani wa halmashauri  hiyo Mbaruku
ally Mgaywa na Lucas Kiberenge wamesema kuwa wamefikia maazimio  hayo baada ya kuona kuwa ofisi ya mkurugenzi
mtendaji inashindwa kumuwajibisha meneja
huyo licha kuoneka wazi wazi kuwa kuna ubadhilifu wa fedha za umma zaidi
ya milioni 600
Meneja wa mamlaka
ya maji Safi na Usafi wa mazingira SUWASA Wilayani humo Enginia Benjamini
Briton amesema kuwa amesikitishwa na maamuzi yaliyotolewa katika kikao cha
baraza hilo kwani hakupewa nafasi ya kujibu chochote wala kujitetea kwa
chochote.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya sikonge bwana Peres Magiri amesema kuwa serikali ya wilaya
hiyo haiwezi kumvumlia mtumishi yeyote mzembe
ambae atabainika kula fedha za umma na huku akipongeza maamuzi yaliyotolewa
na baraza hilo.
Hata hivyo baraza
hilo la madiwani limeazimia kumsimamisha kazi Meneja huyo kwa muda
usiojulikana  huku likimuomba mkaguzi wa
ndani kuanza kufanya ukaguzi ili kuweza kubaini upotevu wa fedha zaidi ndani ya
mamlaka hiyo.



TABORA  YA OMBEWA MAFANIKIO

No comments