Urusi yatishia kulipiza kisasi dhidi ya Marekani
Urusi imetishia kutoza ushuru bidhaa za Marekani za thamani ya karibu dola milioni 540 kujibu hatua iliyochukuliwa na Marekani ya kutoza ushuru bidhaa za chuma na Aluminium.
Urusi iliwasilisha hati husika kwenye shirika la biashara duniani WTO. Japan na Uturuki nazo zimetangaza ushuru zaidi ili kulipiza kisasi dhidi ya Marekani. Umoja wa Ulaya unatarajia kufanya uamuzi hadi ifikapo tarehe mosi mwezi ujao.
Hatua ya Marekani ya kuongeza ushuru kwa sasa haitatekelezwa kwa baadhi ya nchi ikiwa pamoja na za Umoja wa Ulaya, lakini imeshaanza kutekelezwa dhidi ya Urusi.
kamanda wa jeshi la posi tabora wilbrod mutafungwa
Post a Comment