Header Ads

Rais aamua kutoa nusu ya mshahara wake




Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ametangaza kutoa nusu ya mshahara wake kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kijamii nchini humo.
Rais Ramaphosa mwenye umri wa miaka 65, ametoa tangazo hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter, leo na kusema fedha hizo zitakwenda kwenye mfuko maalum unaosimamiwa na Wakfu wa Nelson Mandela .
Hata hivyo haijafahamika ni mshahara kiasi gani Rais Ramaphosa anapokea kwa mwezi, ingawa vyanzo vya habari vinadai anapokea zaidi ya dola elfu 20 alizokuwa akilipwa mtangulizi wake, Jacob Zuma.
Afrika Kusini na dunia kwa ujumla mwaka huu inaadhimisha miaka 100 tangu kuzaliwa kwa kiongozi wa kwanza mzalendo wa taifa hilo Hayati Nelson Mandela, kwa kuandaa miradi na matukio mbalimbali ya kumbukumbu hiyo.


Watu 45 wavuta hewa yenye sumu

No comments