Serikali haitapanga ada kwa shule binafsi - Ole
Hayo yamesemwa leo Mei 21, 2018 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, William Tate Ole-Nasha na kutoa ushauri kwa wazazi au walezi kuchagua shule ambazo wanauwezo wa kumudu gharama ili kuepuka usumbufu kwa wanafunzi na wamiliki wa shule hizo.
“Serikali haitajihusisha na upangaji wa ada kwa shule binafsi bali itasimamia viwango vya ubora, taratibu, kanuni na sheria za uendeshwaji wa shule zote nchini lengo la serikali ni kuhakikisha watoto wote wakitanzania wanapata elimu bora kwa manufaa yao na ya Taifa kwa ujumla”,amesema Ole-Nasha.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri huyo amesema kwamba kwa wanafunzi ambao watasoma katika shule binafsi wanakuwa na nafasi ndogo ya kupata mkopo wa elimu ya juu kwasababu wanachukuliwa ni watu wenye uwezo kwakuwa baadhi ya shule za binafsi zinagharama kubwa kuliko ada ya Chuo Kikuu.
Mpaka sasa Nchini Tanzania kuna jumla ya shule za msingi 1432 ambazo zinamilikiwa na watu binafsi na shule za sekondari ni 1250.
Serikali imesema haitaweza kupanga ada elekezi kwa shule ambazo zinamilikiwa na watu binafsi nchini bali itasimamia ubora katika uendeshwaji wa shule hizo ili kusaidia wanafunzi wote nchini wanapata elimu bora.
uchafu kukidheli tabora
Post a Comment