Header Ads

Tetesi za Soka Ulaya IJUMA 18.5.2018

Manchester United walipwa zaidi ya Manchester City mapato ya Ligi ya Premia Uingereza

Manchester United striker Romelu Lukaku celebrates
Manchester United walipata pesa nyingi kuliko mabingwa wa ligi Manchester City kutoka kwenye Ligi ya Premia msimu uliomalizika majuzi, licha ya City kufana zaidi na hata kuweka rekodi.
United, waliomaliza wa pili, walipokea £149.77m, £328,491 zaidi ya City.
United walilipwa pesa zaidi kwa sababu kuna mechi zao mbili zaidi ambazo zilionyesha moja kwa moja kwenye runinga Uingereza - hii ina maana kwamba pesa walizolipwa kutokana na uwanja wao na huduma nyingine zilikuwa £2.26m zaidi.
Kwa jumla, klabu za Ligi ya Premia zilipokea £2.42bn, £2.1m zaidi kuliko msimu uliopita.
United chini ya meneja wao Jose Mourinho mechi zao zilizoonyeshwa kwenye runinga Uingereza msimu huu zilikuwa 28, sawa na zilizooneshwa za Liverpool na Arsenal. Hata hivyo, zilizoonyeshwa za City zilikuwa 26.
Malipo ya jumla kwa klabu hutokana na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kwenye runinga Uingereza (ambayo asilimia 50 yake hugawanywa kwa njia sawa kwa klabu zote. Asilimia 25% ya mapato yaliyosalia hugawanywa kwa kuzingatia mechi ambazo zimeonyeshwa moja kwa moja kwenye runinga, na asilimia 25 kwa kuzingatia nafasi ya klabu kwenye jedwali), mapato kutoka kwa shughuli nyingine za kibiashara na mapato kutoka kwa haki za utangazaji wa mechi kimataifa.

Manchester City celebrate Premier League titleHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionManchester City walimaliza ligi wakiwa na alama 100, ambayo ni rekodi

City walipokea £38.63m kwa sababu ya kushinda ligi, £1.93m zaidi ya United waliomaliza wa pili.
Malipo kwa klabu za Ligi ya Premia 2017-18
Klabu (kwa kufuata nafasi ligini mwisho wa msimu)Idadi ya mechi zilizoonyeshwa moja kwa moja runingani UingerezaPesa zilizotokana na nafasi kwenye ligiMalipo ya jumla
Manchester City26£38.63m£149.44m
Manchester United28£36.69m£149.77m
Tottenham25£34.76m£144.45m
Liverpool28£32.83m£145.90m
Chelsea26£30.90m£141.71m
Arsenal28£28.97m£142.04m
Burnley10£27.04m£119.77m
Everton19£25.11m£128.01m
Leicester12£23.18m£118.17m
Newcastle18£21.24m£123.02m
Crystal Palace12£19.31m£114.31m
Bournemouth11£17.38m£111.25m
West Ham17£15.45m£116.09m
Watford10£13.52m£106.25m
Brighton13£11.59m£107.71m
Huddersfield10£9.66m£102.39m
Southampton16£7.73m£107.24m
Swansea10£5.79m£98.53m
Stoke12£3.86m£98.86m
West Brom10£1.93m£94.67m

No comments