Header Ads

Tetesi za soka Ulaya Juma PILI 13.05.2018

Mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar huenda akajiunga na Real Madrid kulingana na Zidane

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema kuwa huenda mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar, 26, akashirikiana na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. (Goal)
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa wapinzani wao wa London watalazimika kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Harry Kane 24 ili kufadhili ujenzi wa uwanja wao mpya. (Evening Standard)
Parkour: Wakenya wanaoruka kwenye majengo 'kama paka'
Hary Kane
Kocha anayesakwa na klabu za Arsenal na Chelsea Massimiliano Allegri hataki kuhamia katika ligi ya Uingereza bila kupewa fursa ya kuandaa timu ya ushindi na badala yake ameitaka Juventus kufadhili wachezaji wapya iwapo atasalia nchini Itali.
Dikembe Mutombo: Mchezaji wa DRC aliyewazima wapinzani NBA
Hatua ya klabu ya Manchester City kumsaka kiungo wa kati wa Napoli Jorghino imepigwa jeki na kupungua kwa hamu kwa klabu ya Manchester United kumnunua mchezaji huyo wa Itali. (Manchester Evening News)
kiungo wa kati wa Napoli Jorghino
Image captionkiungo wa kati wa Napoli Jorghino
Kocha wa zamani wa Uingereza Sam Allardyce, 63, atajua hatma yake wiki ijayo ya iwapo atasalia kama mkufunzi wa klabu hiyo msimu ujao. (Guardian)
Beki wa kulia wa Uhispania na Arsenal Hector Bellerin, 23, anasema kuwa atasalia katika klabu ya Arsenal mwisho wa msimu huu. (Sky Sports)
Beki wa kulia wa Uhispania na Arsenal Hector Bellerin, 23,
Fiorentina haina shinikizo lolote la kifedha kumuuza mshambuliaji wake raia wa Itali mwenye umri wa miaka 20 Federico Chiesa, anayelengwa na Tottenham na Chelsea. (Sky Italia, via Calciomercato)
Klabu za Borussia Monchengladbach na RB Leipzig ziko tayari kumsajili mshambuliaji wa Liverpool mwenye urmi wa miaka 18 Rhian Brewster, ambaye alishinda kombe la dunia la vijana wasiozidi umri wa miaka 17 na Uingereza (Mirror)
mkufunzi David WagnerHaki miliki ya pichaREX FEATURES
Klabu ya Huddersfield Town iko tayari kuanza mazungumzo ya kuandikisha kandarasi na mkufunzi David Wagner.
Raia huyo wa Ujerumani alipewa marupurupu ya £2.5m kwa kuifikisha Huddersfield katika ligi ya premia(Telegraph)
Wolves inatumai kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Musa kutoka Leicester, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 akiwa na klabu ya CSKA Moscow kwa mkopo. (Sabah, via Birmingham Mail)
Emmanuel Petit
Image captionEmmanuel Petit
Mchezaji wa zamani wa Arsenal Emmanuel Petit haamini kwamba wachezaji wenza wa zamani Patrick Vieira ama Mikel Arteta wako tayari kumrithi Arsene Wenger kama mkufunzi wa Gunners. (RMC, via ESPN)
Mkufunzi wa Crystal Palace Roy Hodgson anasema kuwa anamtaka winga wa Ivory Coast Wilfried Zaha, 25, kusalia katika klabu hiyo (Talksport)
Mkufunzi wa Newcastle Rafael BenitezHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez
Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anataka kupewa nguvu wa kuamua kuhusu wachezaji atakaonunua msimu ujao. (Mail)
Beki wa zamani wa Marekani Alexi Lalas anasema kuwa uhamisho wa mshambuliaji wa Uingereza wa zamani Wayne Rooney kutoka klabu ya Everton hadi DC United kunaweza kusababisha matatizo katika klabu hiyo. (Talksport)
Juventus imemtambua beki wa Colombia na PSV Eindhoven Santiago Arias, 26, kama mchezaji anayelengwa sana na klabu hiyo msimu ujao(Calciomercato)
Mkufunzi wa Leicester City Claude Puel anatarajia kununua wachezaji wapya katika kikosi chake mwisho wa msimu huu huku idadi kubwa ya wachezaji waliopo wakitarajiwa kuondoka(Leicester Mercury)

No comments