Header Ads

Watu 26 wauawa katika shambulio Burundi

Usalama umeimarishwa Burundi kufautia shambulio ambapo watu 26 wameuawa kaskazini magharibi mwa taifa hilo
Serikali ya Burundi inasema kuwa watu 26 wameuawa wakati wa shambulio kaskazini magharibi mwa taifa hilo.
Ghasia hizo zinajiri siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni iliokumbwa na utata ambayo huenda ikaongeza muda wa kutawala wa rais wa taifa hilo.
Kulingana na mwandishji wa BBC, waziri wa usalama nchini humo Alain Guillaume Bunyoni alisema kuwa wale waliotekeleza shambulio hilo walikuwa ni magaidi kutoka nchini jirani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Amesema baadhi ya waathiriwa waliojeruhiwa wamepelekwa hospitalini ambapo wanatibiwa. Ameongezea kuwa mazungumzo yanaendelea na mamlaka ya DRC kwa lengo la kuwakamata washukiwa wakamatwe.
Walioshuhudia wanasema kuwa washambuliaji hao waliingia nyumba baada ya nyumba usiku wakiwapiga risasi watu na kuwadunga visu mbali na kuchoma nyumba zao.
Ramani ya taifa la Burundi likipakana na jirani zake wa DR Congo na Rwanda
Image captionRamani ya taifa la Burundi likipakana na jirani zake wa DR Congo na Rwanda
Kuna uwezekano kwamba shambulio hilo ni jaribio la kuvuruga kura ya maoni yenye utata iliopangiwa kufanyika wiki ijayo-ikiwa ni mradi wa serikali unaoweza kumfanya rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi 2034.
Makubaliano ya amani yaliositisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi yamezuka upya huku makundi ya upinzani yakijipanga nje ya taifa hilo.

No comments