Header Ads

Qur'an na Biblia Tukufu kutozwa kodi














Serikali ya Uganda imeagiza kuanzia sasa vitabu vitakatifu vya Biblia na Quran vinavyoingizwa nchini humo vilipiwe kodi.

Viongozi wa Kidini kutoka madhehebu hayo mawili makubwa nchini humo wamepokea uamuzi huo kwa tahadhari kubwa na mshangao huku wakisisitiza kwamba, vitabu hivyo vya kidini havipaswi kutozwa kodi kwani vinatumika kujenga na kuimarisha imani za kiroho za wananchi wa Uganda.
Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislaam Nchini Uganda, Ramadhan Mugalu, ameikosoa serikali kwa kusema kuwa, hatua hiyo imevuka mipaka, na kuhoji inawezaje kutoza kodi neno la Mungu?
Kwa upande wake Kamishna wa Makanisa nchini humo, Mchungaji Joram Kahenano, amesema Kanisa lake litalazimika kuongeza bei ya Biblia moja kutoka shilingi za Uganda elfu tatu hadi elfu 18 ili kufidia gharama za kodi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor, uamuzi huo umetolewa baada ya miezi kadhaa ya majadiliano kati ya Mamlaka ya Kodi na Taasisi za Kidin

No comments