Header Ads

Magufuli kuwakabidhi Kombe Simba



Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi, kwenye mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara kati ya mabingwa Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Jumamosi hii ambapo atawakabidhi Simba taji lao.
Hilo limebainishwa mchana huu na Rais wa shirikisho la soka nchini Wallace Karia, ambaye ameweka wazi kuwa wao kama shirikisho wameona ni vyema kumwalika Rais Magufuli kwenye tukio hilo maalum na muhimu kwenye mchezo wa soka nchini.
''TFF kwa kupitia Ofisi ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, tumetuma ombi kwa Mh. Rais Magufuli kwaajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo huo ili awakabidhi Simba taji la ubingwa na tunaamini atakubali'', amesema.
Mchezo huo utapigwa jumamosi hii kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia majira ya saa 10:00 jioni ambapo utatanguliwa na shamra shamra za ubingwa na baada ya mechi Simba watapewa rasmi kombe lao.
Simba mpaka sasa ina alama 68 baada ya mechi 68 huku Kagera Sugar ikiwa na alama 31 baada ya mechi 28 ikiwa katika nafasi ya 10 kati ya timu 16 zilizoshiriki ligi kuu msimu wa 2017/18

No comments