Header Ads

Timu inahitaji mashabiki – Nadir Haroub ‘Cannavaro’




Kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho baina ya Yanga dhidi ya Rayon Sports, beki kisiki, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kuwa timu hiyo inahitaji mashabiki kama mashabiki wanavyo hitaji wanavyowahitaji hivyo sehemu pekee ambayo wanaweza kukutana ni uwanjani.
Yanga ambayo ndiyo wawakilishi pekee kwenye michuano ya kimataifa watashuka dimban la Taifa jijini Dar es salaam Mei 16 kuwakaribisha Rayon Sports ya Rwanda ikiwa ni mchezo wao wa pili wa kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya makundi.

Kwenye mchezo uliyo pita Yanga wakiwa ugenini Algeria walikubali kipigo cha mabao 4 – 0 dhidi ya USM Alger huku wenzao Rayon wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Amahoro jijini Kigali Rwanda ilitoka sare ya goli 1 – 1 mbele ya Gor Mahia FC  hivyo wawawkili hao wa Tanzania watalazamika kushinda mechi hiyo ili kujiweka vizuri kwenye hatua hiyo ya makundi.
Kuelekea mchezo huo tayari viingilio vimeshatajwa ambapo VIP A itakuwa Tshs 15,000, VIP B na C ni 7000 na mzunguko itakuwa ni Tshs 3000 pekee.

No comments