Wanahabari wa kigeni wawasili Korea Kaskazini kushuhudia kuharibiwa kwa eneo la nyuklia
Zaidi ya waandishi habari 20 kutoka nchi za magharibi na China wamewasili Korea Kaskazini leo kushuhudia kufungwa kwa kituo cha kufanyia majaribio ya kinyuklia.
Korea Kaskazini imewaalika wanahabari hao wa mataifa ya kigeni kushuhudia kuharibiwa kwa kituo cha Punggye wiki hii.
Wataalamu wa masuala ya kiufundi hata hivyo hawajaalikwa kuhakiki zoezi hilo huku Marekani ikitaka maeneo ya kufanyia majaribio ya kinyuklia nchini Korea Kaskazini kufungwa kabisa na kuweza kukaguliwa vilivyo kuthibitisha maeneo yote na silaha zote za kinyuklia nchini humo zimeharibiwa.
Uhusiano kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambao ulikuwa umeimarika katika wiki za hivi karibuni umeonekana tena kuzorota baada ya Korea Kaskazini wiki iliyopita kutishia kutohudhuria mkutano wa kilele unaotarajiwa tarehe 12 mwezi ujao kati ya Rais Donald Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
TENOLOJIA YA KUA DUNIA
Post a Comment