Header Ads

Wazee wa Simba wamuomba JPM aiwajibishie Simba



Wazee wa klabu ya Simba wamemuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli awapeleke wakaguzi wa mahesabu ndani ya klabu hiyo ili waweze kukagua masuala ya mahesabu pamoja na kupitia sheria mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zimekaa kibaguzi katika michezo.

Tamko hilo la wazee hao limetolewa leo Mei 18, 2018 zikiwa zimebakia siku mbili kutoka sasa kufanyika kwa mkutano mkuu wa mabadiliko ya kikatiba ndani ya Simba jambo ambalo limeonekana wazee hao kulipinga na kudai mkutano huo ni batili kwasababu viongozi wa klabu hiyo wamekwisha ibadili Katiba wao peke yao na wanachotaka ni wanachama sio mawazo yao.
Mbali na hilo, wazee hao wameendelea kupiinga rasimu ya Katiba ya klabu hiyo toleo la mwaka 2016 wakidai imepitishwa kinyume na sheria za nchi huku wakitaka itambulike Katiba ya mwaka 2014.
Msilize hapa chini mwandishi wetu Crispin Haule 'Kiberenge' akielezea vizuri sakata hilo la wazee wa Simba lililotokea leo.



UCHAFU KUKIDHELI TABORA ANGALIA HAPA CHINI

No comments