Header Ads

Wito umetolewa kwa wanawake mkoani tabora kujitoa katika kumtumikia mungu



Wito umetolewa kwa wanawake mkoani tabora kujitoa katika
kumtumikia mungu na kumfanya wakwanza katika maisha yao 

Hayo yameelezwa na akina mama waliohudhulia katika siku ya
mwisho ya ya kongamano la watumishi wa mungu lililofanyika kwa siku tatu
mfululizo katika kanisa la effeso baptist lililopo bomba mzinga  ambapo muitikio wa wanawake umeonekana kuwa
mdogo ukilinganishwa na wanaume

Aidha vijana wote wametakiwa kujitoa kwa kazi ya mungu ili
kutengeneza taifa linalomcha mungu kwani kundi hilo linakubwa na changamoto
nyingi zinazowatenga na mapenzi ya mungu

Kwaupande wao wachungaji waliohudhuria kongamano hilo
wamewataka watumishi wote wa mungu kuitikia wito popote pale ambapo wataombwa
kuwepo ili kuweza kujifunza zaidi kwani mungu hupitia kwa mwanadam kufikisha
kile alichokusudia 
Hata hivyo wameshukuru ujio wa wageni walioongoza kongamano
hilo kwa siku tatu ambao ni pastor herb monroe, raymond clark barry na lynn
monroe wote kutoka nchini marekani kwa kusema kuwa wamebarikiwa sana.

Kongamano hilo liliandaliwa na kanisa la effeso baptist kwa
kushirikiana na radio uhai fm likiwa na lengo la kuwakutanisha watumishi wa
mungu katika kuimarishana kiimani



NILIANGUKA NA UNGO WA KICHAWI  KANISANI 

No comments