Mashambulizi ya angani yawaua wapiganaji 12 Syria
Shirika la kutetea haki za binadamu Syria lenye makao yake Uingereza limesema mashambulizi hayo yamefanywa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani katika eneo la kusini mwa Albu Kamal ambalo mara kwa mara limeshuhudia mashambulizi ya wanamgambo wenye itikadi kali wa kundi la Dola la Kiislamu IS.
Mkuu wa shirika hilo la kutetea haki za binadamu Rami Abdel Rahman amesema magari matatu pia yaliharibiwa katika mashambulizi hayo yaliyosababisha vifo vya wapiganaji 12 ambao si raia wa Syria. Hata hivyo Abdel Rahman hakutoa maelezo zaidi kuhusu uraia wa wahanga hao.
Jeshi la Marekani limekanusha kuhusika na shambulizi hilo. Msemaji wa kamanda wa jeshi la Marekani Kapteni Bill Urban amesema hawajafanya operesheni yoyote ya kijeshi dhidi ya majeshi ya Syria wala wapiganaji watiifu kwao na wala hawana ripoti za kuthibitisha kutokea kwa mashambulizi.
IS bado yadhibiti maeneo kadhaa Syria
Dola la Kiislamu IS limepoteza sehemu kubwa ya ngome zake nchini Syria tangu mwaka jana lakini bado linaendelea kudhibiti maeneo kadhaa ya jangwani na wanamgambo hao wa IS wamekuwa wakiwashambulia wanajeshi wa serikali na wapiganaji wanaowaunga mkono katika kipindi cha majuma ya hivi karibuni.
MAJAMBAZI 12 SUGU WA KAMATWA TABORA
Post a Comment