Lissu atoa kauli ya kurudi Tanzania
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amefunguka kwamba atarudi nchini siku atakayopona kwani Ulaya siyo kwao na kwa umri alionao hataweza kujifunza namna ya kuishi katika nchi za huko.
Lissu ameyasema hayo kupitia video fupi iliyorekodiwa na Mtanzaia Damian aishiye Uholanzi ambaye alikwenda kumuona katika hospitali aliyolazwa huko nchini Ubelgiji.
Lissu ameeleza kuwa kwa sasa anachosubiri ni kufanyiwa oparesheni moja itakayofanywa mwezi ujao na baadae ataanza matibabu ya kufanya mazoezi ya viungo na baada ya matibabu hayo yote wataweza kurejea nchini.
Lissu amesema kuwa ni lazima atarudi nchini Tanzania kwa kuwa umri alionao kwa sasa siyo umri wa kuanza kujifunza namna ya kuishi katika nchi hizo za ulaya ikiwa ni pamoja na kuhangaika kutafuta kazi.
Mbali na hayo Mbunge huyo ametoa ahadi kwa watanzania kuwa hatakuwa na cha kuwalipa pindi atakaporudi Tanzania bali atajitahidi kwa kadri yoyote ili kuhakikisha anatoa uwakilishi unastahili watanzania.
Post a Comment