Header Ads

Polisi zaidi ya 20 wauawa katika mlipuko Indonesia

mediaPolisi wakipiga doria katika mji wa Surabaya baada ya shambulio kwenye makao makuu yao, Mei 14, 2018.Antara Foto/ Didik Suhartono / via REUTERS
Washambuliaji wa kujitoa muhanga walio kuwa kwenye pikipiki walijilipua karibu na kambi ya polisi Surabaya nchini Indonesia. Shambulio hilo limesababisha polisi zaidi ya ishirini kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa, kwa mujibu wa polisi ya Indonesia.
Shambulio hilo linatokea siku moja baada ya mashambulizi mengine yaliyoendeswa dhidi ya makanisa katika mji huo wa pili kwa ukubwa nchini Indonesia.Takriban watu 14 waliuawa katika mashambulizi hayo.
"Kumetokea mlipuko uliosababisha hasara mongoni mwa polisi wetu," amesema Frans Barung Mangera, msemaji wa polisi wa jimbo la Java Mashariki, bila kusema kama polisi hao waliuawa au kujeruhiwa. Akinukuu video za zilizonaswa na mitambo iliyowekwa kwenye kambi hiyo (CCTV), amesema kuwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja walio kuwa kwenye pikipiki walisimama katika kituo cha ukaguzi kilio karibu na kambi hiyo: "Ni wakati huo mlipuko ulitokea."
Siku ya Jumapili mji wa Surabaya ulikumbwa na mfululizo wa mashambulizi yaliyolenga makanisa matatu na kusababisha vifo vya watu kumi na nne.
Mashambulizi hayo matatu yaliendeshwa na watu wa familia moja. Kundi la Islamic State limedai kuhusika na mashambulizi hayo
Masaa machache baadaye, watu watatu wa familia moja waliuawa na wengine wawili walijeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika jengo la ghorofa karibu kilomita thelathini kutoka Surabaya, polisi wamesema.
Maafisa wameripotiwa kufanya jitihada za kuzuia mashambulizi mengine dhidi ya makanisa.
Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililokiri kufanya mashambulizi hayo.
Lakini Afisa wa shirika la intelijensia nchini Indonesia, amesema kundi la Jemaah Ansharut Daulah (JAD) linashukiwa kutekeleza mashambulizi.

No comments