Header Ads

Yanga yachukua maamuzi mangum







Baada ya kukaa naye na kumtathimini kwa takribani wiki mbili, hatimaye klabu ya Yanga imefikia makubaliano ya imemsainisha mkataba kocha wake mpya Mwinyi Zaheri ambaye ni raia wa DR Congo.


Yanga ambayo imepokonywa ubingwa wa ligi kuu na Simba SC, imekubaliana na mtaalam huy o wa ufundi kwa mkataba wa miaka miwili ya kuifundisha Yanga ambayo inacheza makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Zahera amechukua rasmi mikoba ya Mzambia George Lwandamina aliyekuwa kocha mkuu wa kikosi cha Yanga baada ya kuondoka kimyakimya kurejea kwao Zambia katika klabu yake ya zamani, Zesco United.

Zahera ni kocha msaidizi wa timu ya taifa ya DRC, The Leopard na mwenye uzoefu wa kufundisha soka katika bara la Ulaya pamoja na Afrika.
Licha ya kusaini mkataba huo, Zahera ameondoka nchini kwenda kwao Congo kwa majukumu ya kukitumikia kikosi cha timu ya Taifa ya Congo na baadae atarejea nchini kuendelea na Yanga.


UCHAFU KUKIDHELI TABORA ANGALIA HAPA SYLAS TV ONLINE

No comments