Header Ads

Nikifanya hivyo Magufuli atanifunga" - Ray C


Mwanamuziki wa kike bongo ambaye aliwahi kutikisa Afrika Mashariki kwa sauti yake na 
kiuno chake laini, Rehema Chalamila au Ray C, amesema anaogopa kupost picha za utupu
 kama wengine, akihofia kufungwa na serikali.

Ray C ametoa kauli hiyo akiwa nchini Kenya na kuulizwa juu ya wasanii wanaopost  picha za utupu na kwa nini yeye hapost, na kusema kwamba serikali imeona hali ilikuwa mbaya na kuamua kupiga marufuku tabia hiyo, hivyo iwapo atafanya hivyo huenda akafungwa jela.
“Inakuwa too much ndio maana Rais Magufuli kakataza, si unajua baba yetu mkali kidogo!! It was too much, ilikuwa inaanza kwenda mbali, unajua watoto wanaangalia, ingawa watu wanaendelea, nitapelekwa jela na Magufuli nikifanya hivyo”, amesema Ray C.
Msanii huyo yupo nchini Kenya kwa ajili ya kazi zake za muziki, ambapo pia amepata fursa ya kufanya collabo na msanii wa muziki wa injili Papa Denis.

No comments