Header Ads

Fisi AUA watu Igunga mkoani Tabora



MTU mmoja wilayani Igunga mkoani Tabora ameuawa kwa kushambuliwa na fi si na mwingine amejeruhiwa na mnyama huyo.
Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Ziba, Azizi Kombe alimtaja aliyepoteza maisha katika tukio hilo ni Mwajuma Masanja (37) mkazi wa Kijiji cha Iduguta, ambaye alishambuliwa na mnyama huyo sehemu zake mbalimbali za mwili. Mwingine aliyejeruhiwa ni Shija Maneno (35) mkazi wa Kitongoji cha Ipuli Kijiji cha Igumila Kata ya Ziba, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Nkinga na hali yake bado ni mbaya. Mtendaji huyo alisema watu hao walikuwa mtu na mpenzi wake, ambapo walikunywa pombe za kienyeji kwenye kilabu cha pombe kilichopo Kata ya Ziba.

Aliongeza kuwa baada ya kufika saa tatu usiku waliondoka kwenda nyumbani. Alisema wakiwa njiani fisi aliwakuta na kuanza kumshambulia mwanamke kwa kumng’ata sehemu za makalio na tumboni, hali iliyofanya mwanaume amsaidie mpenzi wake huku akipiga kelele za kuomba msaada. Alisema wakati akitoa msaada kwa mpenzi wake huyo, fisi alimng’ata usoni, hivyo aliamua kuachana na mnyama huyo, ambaye aliendelea kumshambulia Mwajuma hadi alipopoteza maisha papo hapo. Muda mfupi baadaye wananchi walifika eneo hilo, wakiwa na baadhi ya askari wa Kituo Kidogo cha Polisi Ziba na kufanikiwa kumuua fisi huyo.

No comments