Header Ads

kamati ya maji ya kijiji cha songambele kataya salawe halmashuri ya wilaya ya shinyanga vijijni inadaiwa kutafuna shiringi milioni 56 za wanakiji baada ya kukusanya mauzo ya maji na kushindwa kuziweka fedha kwenye akaunti ya kijiji na kuamua kuzitumia kwa matumizi.

kamati ya maji ya kijiji cha songambele kataya salawe halmashuri
 ya wilaya ya shinyanga vijijni inadaiwa kutafuna shiringi milioni 56 za wanakiji baada ya kukusanya mauzo ya maji na kushindwa kuziweka fedha kwenye akaunti ya kijiji na kuamua kuzitumia kwa matumizi.



kamati hiyo iliteuliwa na wanakijiji hao kusimamia mauzo ya maji yanayotokana na kisima kirefu tangu mwaka 2013 ili pesa inayopatika iwekwe benki kwajiri ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendereo  lakiniviongozi hao wametafuna pesa zote.

tuhuma hiyo imebainishwa na mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana NGASA  MBOJE  kwenye kikao cha baraza la madiwani kuwa kamati ya maji ya kijiji hicho imekuwa ikitafuna pesa za wananchi na kutoziweka kwenye akaunti ya kijiji ,huku ikiwawasomea wanakijiji mapato hewa

amesema kuwa suala hilo aliligundua mara baada ya kamati ya kudumu ya fedha ,utawala na mipango kwenda kufuatilia mauzo  ya maji hayo na kubaiini ubadilifu mkubwa kwani hakuna fedha yoyote iliyokuwa aikiwekwa kwenye akaunti ya kijiji zaidi ya viongozi hao kuzigawana na kuzitumia kwa matumizi yao binafsi

aidha kufutia ubadhilifu wa fedha hizo .mwenyekiti huyo ameliagiza jeshi lap polisiwilaya kulishughulikia suala hilo kwa kuhakikisha  wnakamati hao wanakamatwa iliwafungweliwe mashitaka ya kula fedha za wanakijiji kinuyme cha utaratibu waliojiwekea ili liwefundisho kwa viongozi wenye tabia kama hiyo

nao baadhi ya madiwani wa halmashauri hiyo SOYA JILALA na MENGI CHARLES wameunga mkono suala hilo la viongozi kukamatwa haraka ili wazirudishe fedha hizo kwani wananchi walikuwa wakinyanunua maji hayo kwalengo la kutunisha mfuko wa kijiji na siyo kwamatumizi ya watu binafsi.

 kwaupande wake mwandisi wa maji wa halmahauri hiyo SILVESTER MPEMBA amesikitishwa kwa kitendo cha kamati hiyo kutafuna fedha za wanakijiji hao kwa madai kamati zote za kusimamia mauzo ya maji kwenye halmashauri hiyo walizipatia semina ya namna ya ku7hifadhi fedha pamoja na kufungua akaunti ya kijiji baadala yake wamezitafuna pesa hizo

No comments