Shambulizi la Orlando sio tu la kutisha, bali pia la hatari
Shambulizi la Orlando sio tu la kutisha, bali pia la hatari
Magaidi siku zote wana angalau malengo mawili pindi wanapofanya mashambulizi. Wanakusudia kuwaua watu wanaowalenga, na pia kuharibu kabisa maeneo ya wazi ya kijamii. Haya ni maoni ya mwandishi wa DW Washington, Ines Pohl
Shambulizi katika klabu ya usiku huko Orlando, Marekani lililowaua kiasi ya watu 50, ni janga ambalo sio tu la kutisha, bali pia la hatari. Katika mwaka huu wa uchaguzi, mshambuliaji huyo wa Orlando huenda
akafanikiwa kwa malengo hayo.
Shambulizi hilo la Orlando limetokea wakati ambapo Marekani imejikuta iko katikati mwa mtihani muhimu
. Marekani ambayo ndiyo kwanza iko mwanzoni mwa mapambano kuhusu swali la nani ataingia katika Ikulu ya
White House kama rais ajaye wa nchi hiyo. Shambulizi hilo limetokea wakati ambapo uchaguzi wa urais umeanza kupamba moto.
Muda mfupi baada ya shambulizi kutokea, wafuasi wa Donald Trump, wameonyesha jinsi gani wangeweza kumaliza kitendo hiki cha ugaidi. Wameandika katika
mtandao wa kijamii wa Twitter wakimpongeza Trump
kuhusu msimamo wake wa kupambana na Uislamu katika mtazamo dhahiri wa dini ya mshambuliaji.
Post a Comment