Header Ads

Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa, Bernard Cazeneuve,amewataka waandaaji wa michuano ya bara la ulaya ya Euro 2016 juu ya kukataza vilevi katika maeneo ya michezo.


Amesema maeneo ya michezo ni nyeti wakati mechi zikichezwa na hata siku moja kabla ya michuano. Tamko hilo limekuja siku tatu baada ya fujo kuibuka kutoka kwa mashabiki wa Marseille ambao walikua wamelewa. Shirikisho la soka barani ulaya,UEFA wameionya England na Urusi kuwa ziko kwenye wasiwasi wa kutolewa katika mashindano ya michuano ya soka barani ulaya mwaka huu,euro 2016 kama mashabiki wao wataendelea kufanya fujo. Michuano hiyo ya UEFA imeomba radhi kwa hali ya utovu wa nidhamu au vurugu zilizojitokeza kati ya urusi na mashabiki wa waingereza huko Marseille 

No comments