Header Ads

Serikali kuwamilikisha wanavijiji silaha za moto





Serikali imesema italiangalia suala la kutoa vibali vya umiliki wa silaha za kujihami dhidi ya wanyama wakali kwa wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za taifa ambao wanaathirika kutokana na wanyama kuvamia makazi yao.
Hayo yamesemwa Bungeni leo, Mei 11, 2018 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Japhet Hasunga na kuongeza kuwa Wizara yake itaangalia mapitio ya sheria na kujaribu kulipatia mkazo jambo hilo.
“Hili suala liliopendekezwa kwamba tutoe silaha kwa wananchi na hasa katika vijiji kuweza kuzimiliki silaha, basi mwenyekiti pale tutakapokuwa tunapitia sheria pamoja na kanuni tutangalia kama hilo litawezekana ili tuone kama linaweza kusaidia.” amesema Hasunga
Naibu Waziri Hasunga aliongeza kuwa serikali inatoa kifuta jasho kwa wananchi waliothirika na wanyama hao.
 “Kifuta jasho kama mwanachi anakuwa ameuawa ni shilingi milioni moja, kama amejeruhiwa ni laki tano na kama ni mazao kuna kiwango chake kutegemea kilomita ambapo shamba lipo”.
 Wakazi wa vijiji na wilaya mbalimbali wanaidai serikali kiasi cha shilingi milioni 828 kama fedha ya kifuta jasho, wakati matukio ya wanyama kushambulia wakazi jirani na hifadhi yamefikia 3509 Nchi nzima.

No comments