Header Ads

Serikali yazuia uonevu kwa wakulima



WAZIRI wa Kilimo, Dk. Charles Tizeba emelieleza Bunge kuwa kitendo cha kununua mazao yakiwa bado shambani ni kuwaonea wakulima.
Unaponunua shambani hata kipimo cha kununua hakipo, mtu anatazama tu shamba anasema hapa nitakupa shilling elfu sitini kumbe mavuno halisi yatakayokuja kupatikana pale ni shilingi lakini mbili;”amesema wakati anatoa jibu la mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wakati anaomba mwongozo wa Kiti cha Spika, Mbunge huyo alisema, amri ya serikali kuzuia ununuzi wa mazao shambani ni kuingilia uhuru wa mkulima.
Wakati anajibu swali bungeni, Naibu Waziri wa Kilimo, Dk. Mary Mwanjelwa alipiga marufuku uuzaji mazao yakiwa bado shambani. Dk. Mwanjelwa amesema, yeyote atakayekiuka amri hiyo atachukuliwa hastua za kisheria.
“Kwa hiyo tunachokifanya ni kuweka tu utaratibu ambao utahakikisha kwamba mkulima haonewi na mfanyabiashara haonewi, haki bin haki. Wewe kama una shida mkopeshe pesa auze mazao yake ili akulipe pesa lakini kuliko kukadiria kwamba hapa utavuna tani moja kumbe shambani zipo tani tano, una-take advantage ya umasikini wa mtu kumfanyia biashara ambayo siyo halali”amesema Waziri Tizeba na kuongeza kuwa, utaratibu wa masoko utazingatia usawa na haki kwa pande zote mbili.
Awali Dk. Mwanjelwa alilieleza Bunge kuwa, Serikali itasimamia uuzaji mazao ya wakulima kwa njia ya minada ili kuweka ushindani wa bei kumwezesha mkulima apate bei kubwa kama ilivyo kwenye zao la korosho.
Amesema, serikali pia inaendelea kuimarisha mfumo wa uuzaji mazao katika soko la bidhaa za kilimo.


No comments