Header Ads

TETESI YA MICHEZO BARANI ULAYA MEI 2.5.2018

Madrid yatinga fainali ya tatu mfululizo UEFA

Karim Benzema (kulia) alifunga magoli yote mawiliMabingwa wa Ulaya kwa upande wa vilabu Real Madrid imefanikiwa kutinga hatua ya fainali muchuano ya Ligi ya mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kuindosha Bayern Munich ya Ujerumani kwa jumla ya magoli 4-3.

Wakiwa na faida ya magoli 2-1 ugenini, Real Madrid ilihitaji sare ya aina yoyote ili kuweza kutinga fainali ya michuano hii mikubwa kwa upande wa vilabu barani Ulaya.
Joshua Kimmich alianza kufunga kwa mapema kipindi cha kwanza kabla ya Karim Benzema kuisawazishia Madrid baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Marcelo.
Ulikuwa mchuano uliovutia wengi
Image captionUlikuwa mchuano uliovutia wengi
Makosa ya mlinda mlango wa Bayern Sven Ulreich yaliizawadia Madrid goli la pili lililopachikwa na Benzema kabla ya James Rodriguez kusawazisha.
Bayern walikua na nafasi ya kuondoka na ushindi lakini mikwaju ya Corentin Tolisso na Thomas Muller iliokolewa vyema na mlinda mlango Keylor Navas ambaye alikuwa katika kiwango kizuri.
Real itakumbana na Liverpool ama Roma katika fainali itakayopigwa mjini Kiev, Ukraine May 26.
FIFA kuzipa timu za Afrika zinazoshiriki kombe la dunia $2 milioni

FIFA itatoa zawadi ya dola milioni mbili kwa kila mojawapo ya timu tano za Afrika zilizofuzu kucheza kombe la dunia kuzisaidia katika maandalizi, amesema rais wa shirikisho la kandanda barani Afrika CAF.
Offizielles Poster für Fußball-WM in Russland (picture-alliance/dpa/FIFA)
Misri, Morocco, Nigeria, Senegal na Tunisia, zimefaulu kushiriki katika michuano y akombe la dunia itakayofanyika nchini Urusi, na rais wa shirikisho la mpira wa miguu barani Afrika CAF, Ahmad Ahmad, alismea katika taarifa kwamba fedha hizo zitatumika "kushughulikia mapema, suala la bonasi za wachezaji."
Migogoro juu ya malipo katika michuano iliyopita, "ilipelekea kuwepo na hali zilizoathiri vibaya taswira ya soka barani Afrika, ikiwa kwa kiwango kikubwa utendaji wa timu viwanjani," aliongeza.
Mwaka uliopita, shirikisho la kandanda la Nigeria (NFF) lilisaini makubaliano na wachezaji wake wakiahidi kujiepusha na migogoro ya bonasi na malipo ambayo imeharibu kampeni zao za nyuma za kombe la dunia.
Wachezaji wa timu ya Nigeria, Super Eagles walihusika katika mzozo wa muda mrefu kuelekea mashindano ya kombe la shirikisho la mwaka 2013 nchini Brazil, na mgogoro juu ya bonasi pia ukavuruga kampeni yao ya kombe la dunia mwaka 2014.
Matatizo sawa na hayo yameziathiri timu nyingine na bara la Afrika.
Time 32 zinashiriki katika michuano ya kombe la dunia inayofanyika kuanzia Juni hadi Julai, hupokea kitita cha dola milioni 1.5 kila mmoja kutoka FIFA katika mfumo wa malipo ya maandalizi, na zinahakikishiwa kingine kisichopungua dola milioni 8 katika fedha za zawaidi baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.

Mohamed Salah ndiye mchezaji bora wa tuzo ya waandishi wa kandanda



Mohamed SalahHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMohamed Salah

Mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na muungano wa waandishi.
Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne alikuwa wa pili huku mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane akichukua nafasi ya tatu.
Salah, 25, amefunga magoli 31 katika mechi 34 za ligi ya Uingereza akiichezea Liverpoll msimu huu.
Nyota huyo wa Misri - ambaye ndio Mwafrika wa kwanza kushinda taji hilo pia alishinda muungano wa wachezaji wa kulipwa mnamo mwezi April.
Mshambuliaji wa Chelsea na Uingereza Fran Kirby alishinda taji la wanawake la mchezaji bora wa mwaka FWA.
Salah amefunga mabao 43 katika mashindano yote baada ya kusainiwa kwa dau la £34m kutoka Roma mwisho wa msimu.


De Bruyne
Image captionDe Bruyne

Winga huyo wa zamani alifunga mabao mawili katika raundi ya kwanza ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya klabu yake ya zamani katika uwanja wa Anfield.
Kikosi hicho cha Jurgen Klopp kinasafiri kuelekea Stadio Olimpico siku ya Jumatano kwa marudio ya raundi ya pili kikiongoza 5-2 dhidi ya Wataliano hao.
Salah na De Bruyne walipata 90% ya kura kutoka kwa wanachama wa muungano wa waandishi wa kandanda lakini Salah akashinda kutokana na mabao yake mawili aliyofunga dhidi ya Roma wiki iliopita.
Wachezaji wengine waliotarajiwa kupata kura kutoka kwa FWA ni: Sergio Aguero (Man City), Christian Eriksen (Tottenham), Roberto Firmino (Liverpool), Nick Pope (Burnley), David Silva (Manchester City), Raheem Sterling (Man City) na Jan Vertonghen (Tottenham).

No comments