Header Ads

Mrisho Ngassa atoa neno kwa Yondani




Nyota wa zamani wa klabu ya Yanga ambaye kwasasa anachezea Ndanda SC, Mrisho Ngassa, amesema kitendo alichofanya mlinzi wa Yanga Kevin Yondani cha kumtemea mate mlinzi wa kushoto wa Simba Asante Kwasi sio kizuri lakini kilitokana na ukubwa wa mchezo.


Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa 'Instagram' Ngassa ametoa uchambuzi wa baadhi ya matukio ambayo yalitokea katika mchezo huo na kueleza kuwa tukio la Yondani lilitokana na ukubwa wa mchezo ambapo wachezaji hujikuta wakifanya vitu ambavyo hawakutegemea.
''Kweli kitendo ambacho kafanya Yondani sio kizuri lakini angalia mechi ilikuwa ya uzito kiasi gani, hayo katika mpira yapo, haswa mpira wa ushindani kama wa jana'', ameandika.
Kwa upande mwingine Ngassa amezungumzia tukio la Emmanuel Okwi kukabiliana na mlinda mlango wa Yanga Youthe Rostand, kuwa halikuwa la kiungwana kwani alimuumiza golikipa.
''Ukija kwa Okwi kampiga kipa ambae kadaka mpira mfano angemvunja mguu lakini yote ile ni mbinu zakuogopwa uwanjani hicho ndio kiliwapa Simba ushindi kwani kipa alishagongwa akawa anaogopa kwenda'' ameongeza.
Aidha Ngassa amewataka mashabiki kutambua kuwa wao hubaki wanaongea tu kishabiki lakini kwa wachezaji hukutana na kuombana radhi. Pia amewapa hongera Simba kwa ushindi huku akimpa pole Asante Kwasi.

alicho kisema mpoki cha timia angalia hapa sylas tv

No comments