BABA ABAKA MTOTO WA DARASA LA PILI MKOANI SHINYANGA
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia Amos Meshack (36) anayejihusisha na shughuli ya kufinyanga udongo wa pemba kwa tuhuma ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 9 mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Ndala A manispaa ya Shinyanga.
Akisimulia kuhusu tukio hilo lililotokea jana Aprili 30,2018 majira ya saa saba mchana, mama mzazi wa mtoto huyo amesema alibaini mwanae amebakwa baada ya kuona nguo zake za ndani zikiwa zimefichwa nyuma ya kitanda huku chupi ikiwa na damu pamoja na mbegu za kiume na yeye kuonekana kuwa hana furaha na mnyonge.
“Nilimbana mtoto akasema amekuwa akifanyiwa hivyo mara kwa mara akipewa pipi na mwanaume huyo, nilitoa taarifa polisi pamoja na kwa Mwenyekiti wa mtaa kisha tukaenda eneo la tukio kumkamata mtuhumiwa ”, ameeleza mama huyo akizungumza .
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule amesema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili ambapo mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumwita mtoto huyo kwa ahadi ya kumpatia shilingi mia mbili kwa ajili ya kununulia maandazi.
“Kutokana na ahadi hiyo,mtoto aliingia katika nyumba/kibanda ambacho mtuhumiwa hukitumia kufanyia biashara ndogo ndogo za kufinyanga na kutengeneza udongo aina ya Pemba ndipo alimkamata na kumbaka akimsisitiza asieleze chochote kwa mtu yeyote”,alieleza Kamanda Haule.
Kamanda Haule amesema wanamshikilia mtuhumiwa na baada ya uchunguzi wa awali kukamilishwa atafikishwa mahakamani.
Post a Comment