BAYERN MUNICH MDOMONI MWA REAL MADRID LEO
Mshambuliaji Arjen Robben wa Bayern Munich ataukosa mchezo wa timu
yake leo ikikipiga dhidi ya Real Madrid katika nusu fainali ya pili ya
Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Bayern Munich wanaingia katika mchezo huo wakionekana vibonde dhidi
ya Real Madrid ambao wapo mbele kwa mabao 2-1, ushindi walioupata katika
mchezo wa awali.
Cristiano Ronaldo wa Real Madrid amefunga mabao 9 dhidi ya Bayern
Munich, licha ya kuwa mchezo uliopita hakufunga lakini anatarajiw akuwa
hatari katika mchezo wa leo.
Hakuna timu ambazo zimekutana mara nyingi katika Champions League
kama Real Madrid na Bayern Munich, hadi hizi sasa zimekutana mara 26,
Bayern Munich ikishinda mara 11 huku Real Madrid ikishinda 12.
Uwanja wa Santiago Bernabeu ndiyo mahala pachungu zaidi kwa wapinzani
katika Champions League, katika dimba hilo Real Madrid wamefunga katika
michezo yao 41 ya mwisho ya CL na mechi pekee waliyoshindwa kufunga
ilikuwa dhidi ya Barcelona mwaka 2011.
Mbaya zaidi kwa Bayern Munich ni kwamba wanakwenda ugenini katika
kipindi ambacho wamecheza michezo 13 ya Champions League ya ugenini na
yote wameruhusu bao, huku mshambuliaji wao tegemezi Robert Lewandowski
akiwa hajafunga katika mechi 4 zilizopita za CL.

Post a Comment