Header Ads

Kesi dhidi ya mchungaji wa kimarekani yarindima tena Uturuki


Image result for andrew brunson


Kesi dhidi ya mchungaji wa kikristo kutoka Marekani Andrew Brunson imeanza kusikilizwa tena nchini Uturuki akikabiliwa na kifungo cha hadi miaka 35 ikiwa atapatikana na hatia katika mashtaka ya ugaidi na ujasusi yanayomkabili.Kesi hiyo imelaaniwa na Marekani. 

Bruson ambaye ni kiongozi wa kanisa dogo la kiprotestanti katika mji wa Magharibi mwa Uturuki wa Izmir linaloitwa Yenidim Dirillis yaani ufufuo na ambaye anatajwa na rais wa Marekani Donalt Trump kuwa mtu muungwana alikamatwa Oktoba mwaka 2016. 

Waendesha mashtaka nchini Uturuki wanamtuhumu mchungaji huyo kuendesha shughuli kwa niaba ya kundi linaloongozwa na ulamaa wa kiislamu anayeishi uhamishoni Marekani Fethullah Gullen ambaye Uturuki inasema kwamba ndiye aliyehusika kupanga mapinduzi yaliyoshindwa dhidi ya serikali mwaka 2016,pamoja na chama cha wakurdi cha PKK. Vugvugu la Gullen na chama hicho cha PKK ni makundi yaliyopigwa marufuku nchini Uturuki yakitajwa kuwa makundi ya kigaidi.

Mchungaji Brunson anayeishi na kufanya kazi Uturuki kwa zaidi ya miongo miwili pia anatuhumiwa kuwa jaasusi wa kisiasa na kijeshi.

ANGALIA HAPA CHINI



No comments