Header Ads

Israel yasema itamuua Rais Assad

Image result for Israel


Waziri mmoja aliyeko katika kamati ya usalama ya baraza la mawaziri nchini Israel amesema leo kwamba nchi hiyo inaweza kumuua rais Bashar al Assad na kuipindua serikali yake madarakani ikiwa Iran itatumia ardhi ya Syria kufanya mashambulizi yake dhidi ya Israel. 

Waziri wa nishati Yuval Steinitz amenukuliwa na mtandao wa habari wa Israel wa Ynet akisema kwamba Israel haijajiingiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria hadi kufikia sasa,lakini ikiwa rais bashar al Assad ataendelea kuiruhusu Iran kuendesha shughuli zake katika ardhi ya nchi hiyo Israel itammaliza na kuundowa madarakani utawala wake.

Kadhalika waziri huyo ameendelea kueleza kwamba ikiwa rais Assad atairuhusu Iran kuigeza Syria kambi ya kijeshi dhidi ya Israel anapaswa kufahamu kwamba huo utakuwa mwisho wake.

ALICHO KISEMA JOT BAADA YA 
NYUMBA YAKE KUWEKEWA X

No comments