Header Ads

Mchele wapanda bei




BUNGE limeelezwa kuwa, katika mwaka 2017/2018 bei ya mazao makuu ya chakula hasa mahindi, maharage na mchele zimeshuka na kupanda kwa viwango tofauti ikilinganishwa na msimu wa 2016/2017.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma.
Amesema bei gunia la mchele la kilo 100 iliongezeka kutoka wastani wa shilingi 174,316 msimu wa 2016/2017 hadi shilingi 195,201 msimu wa 2017/2018 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 11.98.
"Ongezeko hilo la bei ya mchele linatokana na ongezeko la mahitaji kwa zao hilo ikilinganishwa na uzalishaji wake" amesema Waziri Mwijage.
Amesema, kwa wastani be ya gunia la mahindi la kilo 100 ilipungua kutoka shilingi 98,077 hadi 49,386 ikiwa ni sawa na upungufu wa 49.65%.
“Bei ya jumla ya maharage kwa gunia la kilo 100 ilishuka kutoka shilingi 178,070 mwaka 2016/2017 hadi kufikia shilingi 169,771 mwaka 2017/2018, sawa na upungufu wa asilimia 4.66” amesema Mwijage.
Amewaeleza wabunge kuwa kushuka kwa bei za mahindi na maharage kumesababishwa na ongezeko la uzalishaji kwa kutokana na hali ya hewa nzuri mwaka 2017/2018.

No comments