Header Ads

Mchezaji wa Simba agoma kuongeza mkataba






Kiungo wa vinara wa ligi kuu soka Tanzania bara SimbaSC, Said Hamisi Ndemla, amesema haongezi mkataba wa kuichezea timu hiyo baada ya mkataba wake kumalizika na ataenda kucheza soka la kulipwa kwenye klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden.

Mkataba wa Ndemla na Simba umemalizika April 30 na yeye mwenyewe hataki tena kuendelea kuchezea timu hiyo na anataka kutimiza ndoto na mipango yake ya kucheza soka nje ya Tanzania akiwa tayari ameshafuzu majaribio na klabu ya AFC Eskilstuna.
''Nimemaliza mkataba na Simba na sidhani kama nitaongeza mana nahitaji kucheza soka nje ya Tanzania na ndio muda wa mipango yangu hiyo kutimia nikiwa kama mchezaji huru tofauti na nikiwa na mkataba mpaka timu iamue kuniuza,'' amesema.
Kwasasa Ndemla atalazimika kusubiri hadi msimu ujao ili kuanza kucheza Ligi Kuu ya Sweden kwa kuwa dirisha la usajili limeshafungwa na msimu unaelekea ukingoni. Awali Ndemla alifuzu majaribio lakini timu hiyo ikawa inamtaka kwa mkopo jambo ambalo Simba hawakuafiki.
Ndemla aliisaidia Simba kwenye mechi kadhaa msimu huu ikiwemo ule mchezo dhidi ya Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba ambapo alifunga bao moja na kusaidia moja katika ushindi wa mabao 2-0.

No comments