Header Ads

Katibu Mwenezi CCM auawa kwa kupingwa risasi




Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi, CCM Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Ndg. Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.
Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi, CCM Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Ndg. Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kuwa Bw. Chapewa alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana wakati akiwa anakunywa pombe katika moja ya baa anayomiliki kijijini hapo.
Kamanda Kyando amesema kuwa Chapewa ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Mwandui iliyopo mwambao wa bonde la ziwa Rukwa alimiminiwa risasi na watu hao kwa kutumia bunduki aina ya gobore kisha kumkata kata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.
Hata hivyo amesema kwamba amesema baada ya wauaji kutekeleza adhima yao waliondoka kuelekea kusikojulikana na hawakuchukua kitu chochote kutoka kwa marehemu wala katika baa hiyo.
Kamanda Kyando amesema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea kufanyika na watuhumiwa wanasakwa popote walipo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.
MBUNGE MSUKUMA WA TETEA WA SANII WA TANZANIA
ANGALIA HAPA SYLAS TV

No comments