Header Ads

Niyonzima aweka rekodi TANZANIA


Baada ya klabu ya soka ya Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara kwa msimu wa 2017/18, nyota wa timu hiyo Haruna Niyonzima amekuwa mchezaji wa kwanza kutwaa ubingwa huo mara nne mfululizo.

Niyonzima ambaye msimu uliopita aliichezea Yanga na kutwaa ubingwa huo kwa mara ya tatu mfululizo, msimu huu tena amefanikiwa kuchukua akiwa Simba na kuweka rekodi hiyo ya kipekee kwenye soka la Tanzania.
Nyota huyo raia wa Rwanda hajawa na msimu mzuri sana ndani ya Simba kutokana na kusumbuliwa na jeraha la kidole kwenye mguu wa kulia, lakini sasa ameshapona baada ya kufanyiwa matibabu nchini India na huenda msimu ujao akaitumikia timu yake ipasavyo.
Kwa upande mwingine Niyonzima anaweza akaonekana kwenye mchezo wa kesho ambapo Mabingwa hao wapya watakuwa ugenini mjini Singdia kucheza na Singida United huku wakijaribu kulinda rekodi yao ya kutofungwa.
Msemaji wa Simba Haji Manara amempongeza kiungo huyo kwa kuandika ''Haruna Niyonzima anakuwa mwanadamu wa kwanza duniani kushinda ubingwa wa Tanzania mara nne mfululizo kwa vilabu viwili tofauti, rekodi hii haijawekwa na yoyote Bongo

No comments