Header Ads

jali ya Mbunge wa CHADEMA ilivyotokea LEO


Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) wa Mkoa wa Singida Mhe . Jesca Kishoa amepata 
ajali Jijini  Dodoma majira ya saa nne asubuhi leo.

Akizungumza na www.eatv.tv kutoa taarifa za awali Afisa Habari wa CHADEMA Bw. Tumaini Makene amesema kwamba Mh. Kishoa amepata ajali asubuhi kwa kugongana na gari ndogo aina ya Pick Up alipokuwa njiani akielekekea kwenye majukumu yake ya kibunge. 
Makene ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea katika njia panda ya Area D mkoani huko.
Hata hivyo ameeleza kuwa kwa sasa Mh. Kishoa yupo katika Zahanati ya Bunge akipatiwa matibabu na uangalizi wa awali na kwamba wanasubiri kupata taarifa za Madaktari ili kujua hatua zaidi.
Kwa upande wa Mume wa Mbunge huyo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila amesema kwamba amepata taarifa za ajali hiyo ya mkewe na kwa sasa yupo Morogoro akielekea Jijini Dodoma kwa ajili ya kumuona mkewe.
Endelea kufuatialia ukurasa huu kwa taatifa zaidi kuhusu hali ya Mbunge huyo 

No comments