Hofu ya mashabiki wa Liverpool yazidi kushika kasi

Timu ya Liverpool jana Mei 02, 2018 ilifanikiwa kutinga hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya baada ya miaka 11 licha ya kupoteza mchezo huo kwa kufungwa magoli 4-2 dhidi ya AS Roma.
Pamoja na kutinga hatua ya fainali lakini mashabiki wa Liverpool wamekua na wasiwasi na kocha mkuu wa timu hiyo Jurgen Klopp kutokana na historia ya matokeo mabovu katika michezo ya fainali.
Mathalani katika michezo ya fainali sita aliyoshiriki kama kocha mkuu wa vilabu vya Borussia Dortmund na Liverpool amefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee.
Fainali ya mwaka 2012 katika kombe Ujerumani ndiyo ulikua mchezo pekee kushinda akiwa na timu ya Borussia Dortmund.
Jedwali linaloonesha matokeo ya michezo ya fainali ya timu za Liverpool na Borrusia Dortmund chini ya kocha Jurgen Klopp.
MWAKA
|
MATOKEO
|
MASHINDANO
|
---|---|---|
2012
| B. Dortmund 5-2 B.munich | Kombe la ujerumani |
2013 | B. Dortmund 1-2 B.munich | Ligi ya mabingwa ulaya |
2014 | B. Dortmund 0-2 B.munich | Kombe la ujerumani |
2015 | B. Dortmund 1-3 Wolfsburg | Kombe la ujerumani |
2016 |
Liverpool 1-4 Man.city (Penati)
Liverpool 1-3 Sevilla
|
Kombe la ligi England
Kombe la Europa
|
Liverpool itakutana na bingwa mtetezi klabu ya Real Madrid katika mchezo wa fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya utakaochezwa Mei 26 katika mji wa Kiev nchini Ukraine
angalia hapa sylas tv
Post a Comment