Header Ads

chezaji wa filamu za ngono Stormy Daniel APEWA dola 130,000 na Donald Trump kuficha siri

Image result for Stormy Daniel

Mwanasheria mpya katika kundi la mawakili wa rais wa Marekani Donald Trump, Rudy Giuliani amesema Trump alimrudishia mwanasheria wake mwingine dola 130,000
 alizomlipa mchezaji wa filamu za ngono Stormy Daniel ambaye anadai alikuwa na uhusiano wa kingono na Rais Trump.
Image result for Stormy Daniel

 Stormy alikabidhiwa fedha hizo na mwanasheria Michael Cohen siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa mwishoni mwa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Donald Trump. 

Akizungumza na kituo cha televisheni cha Foxnews cha nchini Marekani Giuliani alisema malipo hayo hayana uhusiano wowote na kampeni za Trump, na kwamba hayakukiuka sheria yoyote. Hata hivyo, wataalamu wengine wa masuala ya sheria hawakubaliani naye, kwa hoja ya muda na mazingira yalipofanyika malipo hayo. 

Wakosoaji wanaamini Trump aliyekuwa anaandamwa na kashfa nyingine ya kutoa matamshi machafu kuhusu wanawake, alikuwa akitaka kumnyamazisha Stormy Daniels asifichue uhusiano wao, hali ambayo ingeweza kumnyima ushindi.

angali hapa sylas tv kilicho jili



No comments