Caster Semenya aingia fainali 800m
k
Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amefika fainali ya mbio za mita 800m wanawake ambazo zitafanyika Jumapili.
Semenya, 25, aliyeshinda fedha Olimpiki za London 2012, aliandikisha muda wa dakika moja na sekunde 58.17 kushinda kundi lake la nusufainali.
Mkenya Margaret Wambui pia alifika fainali muda wake nusufainali ukiwa 1:59.21.
Mwanariadha wa Burundi Francine Niyonsaba pia atajitosa uwanjani kumenyana na wengine katika mbio hizo baada ya kufuzu, muda wake ukiwa 1:59.59.
Mwingereza Lynsey Sharp pia alisonga, muda wake ukiwa 1:58.65, lakini Mwingereza mwingine Shelayna Oskan-Clarke hakufanikiwa
Post a Comment