Header Ads

CHINA YA TENGENEZA NA RAJA LA VIOO

Daraja refu zaidi la kioo kufunguliwa China

  • Saa 8 zilizopita
Daraja la Zhangjiajie, ChinaImage copyrightAP
Image captionDaraja hilo la kioo litafunguliwa katika mkoa wa Hunan
Daraja refu zaidi duniani ambalo sakafu yake ni kioo litafunguliwa katika mji wa Zhangjiajie katika mkoa wa Hunan nchini China wikendi hii.
Daraja hilo ndilo la juu zaidi lenye sakafu ya kioo duniani na linaunganisha milima miwili ambayo hufahamika kama Milima ya Avatar. Filamu ya Avatar iliandaliwa katika milima hiyo.
Wale wenye ujasiri wataweza kutazama mandhari ya kuvutiaImage copyrightREUTERS
Image captionWale wenye ujasiri wataweza kutazama mandhari ya kuvutia

Daraja kwa tarakimu

Ujenzi ulikamilika Desemba mwaka jana. Urefu wa daraja hilo ni 430m na liligharimu $3.4m (£2.6m).
Daraja hilo limewekwa 300m juu ya ardhi, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Xinhua.
Sakafu yake imeundwa kwa vipande 90 vya vioo ambavyo vina tabaka tatu.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, daraja hilo lenye upana wa mita 6, ambalo mchoro wake uliandaliwa na msanifu mijengo kutoka Israel Haim Dotan, tayari limeweka rekodi kadha za dunia katika usanifu mijengo na ujenzi.
Muonekano wa daraja hiloImage copyrightREUTERS
Je, na usalama wake?
Hili ni suala kuu. Lakini maafisa wameandaa hafla za kudhihirisha uthabiti wake. Maafisa walituma watu wenye nyundo kujaribu kuvunja vioo. Pia magari yaliyojaa abiria yalipita juu yake mapema mwezi huu.
Mwandishi wa BBC Dan Simmons ni mmoja wa walioalikwa kujaribu kubaini iwapo vioo vya daraja hilo vinaweza kuvunjika.
Dan Simmons akipima uwezo wa daraja refu zaidi la kioo duniani
Maafisa walituma watu na nyundo makusudiImage copyrightAP
Image captionMaafisa walituma watu na nyundo makusudi
Magari yaliyojaa watu pia yalipita juuImage copyrightAP
Image captionMagari yaliyojaa watu pia yalipita juu
Maafisa wanasema watu 8,000 wataruhusiwa kutumia daraja hilo kila siku

No comments