Fifa kuwaongeza ujuzi makocha wa Tanzania
KALI ZOTE BLOG
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kwa mara nyingine limeipa nafasi Tanzania kwa kutoa kozi maalumu ya kuwa sawa kimwili kwa makocha wa Tanzania wenye leseni kiwango B.
Kozi hiyo inayoendeshwa na mkufunzi kutoka FIFA, Dk Praddit Dutta, raia wa India itafikia ukomo Ijumaa wiki hii.
Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine ameishukuru FIFA kwa namna inavyoipa nafasi Tanzania katika kozi mbalimbali hususani za ukocha na uamuzi
Amesema kwa kuwa FIFA ina malengo chanya na Tanzania kwa kutoa kozi mbalimbali ikiwamo hiyo ya mwili inayolenga kuwapa ujuzi makocha hao kuwajengea uwezo wachezaji kuwa na stamina.
Amewataka makocha watakaohudhuria kozi hiyo kutumia fursa hiyo ya mafunzo si kwa ajili yao peke yao bali kuendeleza ujuzi huo kwa wengine ambao hawakubahatika kuwa sehemu ya wateule wa FIFA.
FIFA kwa kushirikiana na Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), chini ya Mkurugenzi Salum Madadi, imepitisha majina ya makocha 27 kuhudhuria kozi hiyo inayofanyika jijini Dar es Salaam.
Post a Comment